Zaburi 23 ikisomwa kwa Kiswahili

3 years ago
8

Zaburi 23 ikisomwa kwa Kiswahili
Psalm 23 read in Swahili
Zaburi 23
Mungu mchungaji wangu
(Zaburi ya Daudi)

1 Mungu ni mchungaji wangu,
sitapungukiwa na kitu.

2 Hunipumzisha kwenye malisho mabichi;
huniongoza kando ya maji matulivu,
3 na kuirudishia nafsi yangu nguvu mpya.

Huniongoza katika njia sawa
kwa hisani yake.

4 Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo,
sitaogopa hatari yoyote,
maana wewe ee Mungu u pamoja nami;
gongo lako na fimbo yako vyanilinda.

5 Umeniandalia karamu mbele ya maadui zangu;
umenipaka mafuta kichwani pangu;
kikombe changu umekijaza mpaka kufurika.

6 Kweli wema wako na fadhili zako zitakuwa pamoja nami,
siku zote za maisha yangu;
nami nitakaa nyumbani mwa Mungu milele.

Loading comments...