LISHE BORA NI MTAJI: NIMUHIMU KUWEKEZA KWA WATOTO:

5 months ago
130

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO)
liliamua kufanya kitu kikubwa nchini Tanzania kwa siku ya Chakula Duniani.

Walitaka kuleta mabadiliko katika maisha ya watoto na historia isio futika kwenye maisha na familia zao kwa kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa lishe bora. FAO iligundua kuwa njia bora ya kufanya hivyo ilikuwa kuanzisha programu ya kufundisha watoto mapishi ya vyakula vyenye lishe.

Kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania na wadau wengine wa
maendeleo, FAO ilianza kutekeleza wazo hili la kipekee. Kupitia miradi yake mbali mbali ambayo hutekelezwa nchini Tanzania ilinayo husika na kilimo pamoja na masuala ya lishe kama vile mradi wa AGRI-CONNECT unao tekelezwa katika mikoa ya Tanzan ia bara na Zanzibar, unao husisha shule za msingi.

Stella Kimambo ni afisa lishe kutoka Fao Tanzania, kupitia siku ya chakula duniani ambayo ilifanyika kitaifa Mkoani Kigoma anaewafundisha watoto kuhusu umuhimu wa vyakula vya protini kwa familia na hasa kwa watoto kama anavyo onekana kwenye video hii.
#FAO

Loading comments...